MUNGU ANAPOTAKA KUJIFUNUA KWAKO, ROHO MTAKATIFU ANATABIA YA KUMUANDALIA MAZINGIRA NDANI YAKO NA KUKUANADAA WEWE ILI USTAHIMILI KUUPOKEA UTUKUFU WA MUNGU ANAPOSHUKA KWA KUKUFUNDISHA KUHESHIMU NA KUTUMIA “NGUVU YA MUDA WA TOBA NA UTAKASO.”
Bwana Yesu Kristo Asifiwe!!!
kama Raisi katika maisha ya kawaida kabisa anavyo andaliwa mazingira ya eneo analo taka kwenda,ziara hiyo yawezekana ameombwa kwenda au ipo katika mipango yake. na watu wakumpokea wanavyo andaliwa namna yakustahimili kumpokea na kumfaidi kwa ule ujio wake; vivyo hivyo katika maisha ya kiroho kuna maandalizi.
Ni rahisi sana kumuomba Mungu ajifunue katika maisha yako, lakini ni vigumu sana kwa wengi kuwa na maandalizi au kujua ni namna gani Roho mtakatifu anaachilia fulsa/mwanya wa kujiandaa ili kumruhusu Mungu kujifunua ndani yako wakati atakao yeye.
Swala la utukufu wa Mungu ni kitu binafsi kati ya Mungu na wewe, na wala si kundi hata kama utukufu huo umeshuka kwenye kundi.
Umewahi kujiuliza kwanini watu wengi katika mikutano ya injili, ibada za makanisani au katika matamasha ya kiroho utukufu wa Mungu unaweza kushuka na usiwasaidie kabisa,hata kama mtumishi yupo vizuri, wataouna hapo na wengi nguvu zile zitawadondosaha, ila hawaendi nao popote, mkutano au semina ikiisha na wao wanarejea katika hali ya kawaida.
Au umewahi kujiuliza kwanini Mungu anaweza kushuka sehemu, alafu wewe upo lakini yeye akaondoka kwakusema haupo, Tazama vifungu hivi walau kwa uchache unielewa nacho maanisha; Mwanzo 3:9 Isaya 50:2, 65:12, 66:4 na Ezekiel 22:30.
Moja ya tatizo ni maandalizi yaliyo fungwa ndani ya MUDA wa TOBA na UTAKASO.
Sasa najua Roho mtakatifu ameamua kutuvusha hapo,kwa kutusaidia kujua na kutumia NGUVU iliyomo ndani ya Muda wa Toba na Uatakaso..
Fuatana na mimi utaelewa zaidi.
Matendo 3:19 TUBUNI basi (mrejee) MKAMGEUKIE Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana
Toba tunafanya ili kugeuga kama tupo katika njia isiyo sawa basi turejee kwa Bwana, na toba hiyo inabebwa sana na muda.wengi wanaweza kuwa hawajui hilo mana lazima ujue ukicheza na toba unacheza na ufalme wa mbinguni, vitu hivi viwili vinabebwa na muda
Tazama Mathayo 3:2“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu (muda).”
Utakaso tunaufanya kwa lengo la kuwekwa wakfu kwa kazi ya Bwana, tunafanya kwa kututenga rasmi kwa kazi au mazungumzo na Bwana, tunafanya kwa kuweza kustahimilishwa walau kuuona utukufu wa Mungu na kusikia anaujumbe gani kwetu, lakini zaidi kustahimili kuupokea kilicho bebwa ndani ya utukufu huo kila siku ajifunuayo ndani yetu.
Lengo la utukufu wa Mungu kushuka;
ni kukuvusha eneo ulilo kwama au kukupeleka eneo lililokusudiwa. Ni ishara/alama kwamba nguvu za Mungu zipo na wewe, ulionekana ukivusha watu mto yordani…jifunze pia uhusiano uliopo kati ya Yoshua 3:5 na Yoshua 7:13….utukufu huu uliwavusha hawa ndugu, haukuwavusha tu ukakoma la! Ila ulikuwa pamoja nao, ila walipotenda dhambi utukufu wa Mungu ukaondoka, wanao jua kupima mizani ya kiroho walipoona haupo wakamuuliza Mungu kosa liko wapi, walipo liona kosa na kutengeneza kwa kuheshimu muda wa toba na utakaso ambao ulihusisha KABILA,JAMAA,FAMILIA HADI MTU BINAFSI, utukufu ukarejea na wakazidi lutembea na Mungu. Ni kitu cha mtu binafsi hatakama kimeshuka kwa watu wengi.
Kuna vitu vinadhihirisha kuwa hapa utukufu wa Mungu niliye anzanao upo, umepungu,umeongezeka au umeondoka kabisa… ukijua kutumia muda wa toba na utakaso inakusaidi kujua tatizo ni nini na nini la kufanya. Tazama Yoshua 3:5,7:13, Kutoka 19:10, 24:16 13:21, 40:34 1Falme 8:10, Yohana 1:14, Ufunuo 15:8…n.k
Tazama 1:
Kutoka 19:10 Naye BWANA akamwambia Musa, “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu (ukawatakase) LEO NA KESHO…..11 na wawe TAYARI KATIKA SIKU YA TATU, kwa sababu siku hiyo, BWANA atashuka juu ya mlima Sinai machoni pa watu wote.
Hapa Mungu alitaka kujifunua si kwasababu wametenda dhambi la! Ila alitaka kuzungumza nao, Swali linakuja kwanini aliwaambia wajitase ndani ya masaa 48?
Mfano:- umewahi kuwa njiani au kwenye gari,kazini au popote pale gafula unasikia kuomba maombi ya toba na kujitasa? Alafu ukapuuzia au ukasema ntaomba baadae au ntaomba nyumbani au ntaomba kesho, na uwo muda uliopanga wewe ukaomba kiu ya kuomba ikakatika au usiombe kwa shauku na mzigo ambao ulikujia pale ndani?
Sasa najua wengi watasema ningeombaje kazini? Hilo ndio kosa la kwanza kushindwa kujua namna ya kuomba maombi ya namna tofauti mahali tofauti hasa kwa kushindwa kuwa na maana(definition) nzuri ya maombi ni nini.
Kosa la pili litakuja kwa kushindwa kuutumia ule muda, ambao nguvu zake ni matokeo ya nini Mungu alitaka kufanya kwaajili yako, na pia nguvu zake ndio sababu iliyo mfanya Roho Mtakatifu kukuheshimu, kukupenda na kuja kukuandaa..
Tazama 2:
3:5 Ndipo Yoshua akawaambia hao watu, “JITAKASENI, kwa kuwa KESHO BWANA atatenda mambo ya kushangaza katikati yenu.”
Hapa Mungu alitaka kujufunua kwao si kwa mazungumzo la! Ila alitaka kwa kushusha utukufu wake awavushe mto yordani, Swali linakuja kwanini aliwapa masaa 24 ya kujitakasa?Yoshua
Mungu atupi vitu eti kwasababu tu, tulimuomba, ila wakati mwingi anatoa kulingana na mipango aliyo kuwa nayo hasa kuzingati muda aloukusudia. Lakini wewe kupokea ndio hasa inategemea mazingira uliyopo,
Tazama 3:
Yoshua7:13 ‘‘ ‘Nenda, ukawaweke watu (uwatakase) wakfu. Waambie, ‘JITAKASENI mjiandae kwa KESHO, kwa sababu hili ndilo asemalo BWANA wa Israeli: kwamba kitu kilichowekwa wakfu kipo katikati yenu, Ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka mtakapokiondoa.”
Hapa Mungu taifa la Isrel lilienda kinyume na agano walilo weka na Mungu, mmoja wao alipokosea Mungu akanyamaza kimya wakapigwa na adui zao, Yoshua alipoomba toba na kumuuliza Mungu, Mungu akawapa muda wajitakase ili ashuke na alitatue tatizo Swali langu kwanini aliwapa muda ule tena wajitakase?
Jiulize na Wewe!!
1. Je, wasingekuwa wanatumia ndani ya masaa hayo wanayopewa kujitakasa nini kinge kuwa kinatokea? Na kama umeona walau ka upenyo kakujibu swali, umeina nguvu iliyobebwa ndani ya muda huo wa kujiweka wakfu?
2. Kwanini Biblia haijaweka wazi sana juu ya watumishi wa Mungu ambao wamekuwa na mazungumzo na Mungu kila wakati, kama Ibrahimu, Yakobo, Musa, Yoshua….n.k?
Jibu langu fupi tu, ni moja ya vitu ambavyo Mungu amenifundisha; watu hawa walikuwa na uwezo mkubwa sana wakutembea kwa maelekezo ya Roho mtakatifu hasa kwa kuheshimu muda huo wa toba na utakaso.
Kuna maandalizi binfsi ambayo Roho Mtakatifu anamuandaa mtu pale Mungu anapotaka kujifunua kwa mtu huyo pasi kujarisha anajifunua kwa ghadhabu au wema, ila jua hili; ukimpa Mungu nafasi ndani yako, ukakubali kutembea chini ya agano la kristo, utakapo kosea njia kwa kuifuata ile iliyo kinyume na Kristo, Mungu yupo tayari kuingilia kati, au ukiwa chini ya uangalizi wa Kristo,tayari upo kwenye nafasi ya Mungu kujifunua au kukuhudumia wakati wowote apendao; lakini kabla ya hayo mawili kutokea, Roho Mtakatifu anakuandaa kuruhusu hali ya Mungu kuingilia kati.
Lengo langu ujifunze kitu hiki; maandalizi ya Roho mtakatifu huwa yana tazama sana MUDA na sio mazingira, nini Mungu amekusudia kufanya kwako wakati fulani ndiocho kitu kinacho mpa Roho Mtakatifu nafasi ya kuku andaa mapema sana.
@Daniel Mwaitenga