SOMA KISA CHA DADA HUYU:
Dada huyu ambaye kwa sasa kalazwa hospitali takribani mwaka mmoja na miezi kumi na moja sasa anatamani neema ya Mungu imfikie, anaamini kwamba kuna Baraka na nafasi nzuri Mungu kaiandaa ili aje kusema asante Mungu na ashuhudie wapendwa lakini bado changamoto anayo, na pia shetani anataka kujiinua na kumshawishi kwamba Yesu hawezi. Mpendwa simama kwa maombi kwajili yake.
Kihistoria ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 ambae amedumu katika ndoa yake kwa miaka sita sasa, hakujaliwa kupata watoto katika kipindi chote hicho. Alikua ni mtu ambae anamtumikia Mungu yeye pamoja na mume wake.
Kama asemavyo katika maelezo yake
“Changamoto zimeanza pale nilipokaa ndani ya ndoa kwa miaka miwili na kutopata mtoto, familia yangu ilikuwa pamoja nami na kuniombea lakini familia ya mume wangu ilikuwa kinyume kabisa na mimi, kila mgeni aliekuja kutoka kwao alinitusi na alinidhihaki. Kweli nimekuwa nikimlilia na kumsihi Mungu anifungue na kuniondoa katika jaribu hilo. Mume wangu hakunitenga hakunisema vibaya na alikuwa na mimi kila ninapodhihakiwa”.
Baada ya miaka mitatu katika hali ile siku moja nikiwa natoka kanisani nilikuta wageni nyumbani walikuwa ni wifi, shangazi na mamamkwe niliwasalimia kwa amani kabisa lakini hawakunijibu lolote. Pembeni yao alikuwepo mwanamke mwingine ambae sikumfahamu lakini nikapewa taarifa ndo kaletwa kuziba nafasi yangu. Nikaingia ndani nikapiga goti nikamwambia Mungu unalo kusudi la mimi kuwa katika ndoa hii naomba simama kwajili yangu.
Nilipomaliza nilirudi nje na kuwakaribisha ndani ila hawakutaka wakasema wanasubiri hadi mtoto wao arudi. Basi niliendelea na shughuli za uaandaji wa chakula na muda si mrefu mume wangu alifika na kuwasalimia nao walimweleza liliowaleta. Mume wangu alipinga swala hilo sana nao waliondoka wakilaani familia yetu.
Baada ya miezi miwili hali ya kitofauti ikawa inatokea nikawa naota ndoto za ajabu sana kila nikimshirikisha Mume wangu tunaamka na kusali kesho nakuwa vizuri. Tatizo hilo likadumu takribani miezi minne lakini siku moja mamamkwe , shangazi pamoja na dada wa mume wangu walikuja ambapo mumewangu hakuwepo wakaingia ndani, ghafla nikashangaa kila mtu anakaakimya baada ya nusu saa nikajisikia mzito sana kisha dada wa mume wangu akaniambia nipike chakula changu tu lakini cha kaka yao na wao atapika yeye. Niliona haiwezekani hivyo nikamsihi atapika jioni kwani nilishapika chakula cha wote alikataa na kunitolea maneno makali ambayo yaliniumiza sana ila nikajipa moyo kwamba Mungu yu pamoja nami.
Baada ya mume wangu kurudi kutoka kazini aliwakuta ndugu zake na kuwapokea na alihisi ujio wao haukuwa wa heri lakini walionesha furaha kwake. Basi baada ya muda nilitenga chakula na mama mkwe nae akatenga alichokua amekiandaa yeye na Mume wangu akadai hawezi kula sehemu mbili mimi nikamsihi ale cha mama tu afu changu kitaliwa usiku nae akakubali. Baada ya siku tatu nao wakaondoka tukaendelea kuishi vizuri kwa amani na mume wangu.
Baada ya wiki mbili nilijisikia uchovu wa mara kwa mara nikaenda hospitali kupima nini tatizo. daktari akaniambia majibu yanaonesha ninaujauzito kweli nilipiga kigelegele na kumuita Mungu na kusema asante. Baada ya kurudi nyumbani nilimjulisha mume wangu na alifurahi sana na tukapiga goti kumwambia Mungu asante. Baada ya taaarifa kuwafikia ndugu na jamaa na hali ilivyojionesha yakaibuka mengine mama mkwe anadai huyo mtoto aliyeko tumboni ni mzimu anamwambia mume wangu hakuna tunachokisali na kunituhumu mimi ni mshirikina na kumshawishi mume wangu asipokee ujauzito huu. Maswali mengi yakaja kichwani walichokua wanataka nini? Kama ujauzito umepatika tatizo nini tena?
Maishani kuna mengi na yote yanapita,Kwa sasa nipo hospitalini sijajifungua na ninaujauzato upatao miaka miwili sasa nimekua kama picha, kila uchunguzi umefanyika Napata uchungu kama najifungua mara nne kwa wiki nimekua kama sanamu ya watu kuja kuniangalia nimehamishwa hospitali tatu na sasa nasubiri neema ya Mungu tu.
Kinachonisikitisha ni kwamba mume wangu kashanikatia tamaa kachoka kunihudumia nasikia kaoa mke mwingine japo na yeye hajabahatika kupata mtoto lakini amentelekeza hospitali ni ndugu zangu ndo wanonisaidia na kikubwa namshukuru Mungu kwamba wale watumishi wa Mungu niliokua nao pamoja kanisani wamekua mstari wa mbele kuja kunipa faraja.
Ndugu yeyote yule anayekumbuka kumuomba Mungu naomba aweze kuniombea kwani nimeteseka sana. Niombeeni nipone na pia muombee mume wangu na familia yake Mungu aifungue na kuiponya. Sema Neno la rehema kwa Mungu nae atasikia na kunisaidia katika haya.