Shalom wapendwa!! USCF-SAUT Mwanza, tunapenda kukutafakarisha mambo machache wakati tunaelekea tarehe 25/10/2015 siku ya kupiga kura kumchugua lango wa taifa la Tanzania yaani Raisi pamoja na wabunge na madiwani.
Hatima ya Taifa/mwanadamu imefungwa katika nyakati na Majira usipotambuwa wakati na majira ya Mungu juu ya Taifa lako hilo ni tatizo Tunapozungumza kwa habari ya nyakati na majira tuna maana hii; Majira: Ni vipindi mbalimbali ndani ya wakati ulioamriwa; mfano masika, kipupwe, kiangazi, n.k Nyakati: Ni vipindi kulingana na matukio ya makusudi; mfano asubuhi, jioni, nyakati za mwisho, nyakati za utandawazi, wakati wa kupanda, kuvuna, n.k Ni muhimu sana kufanya kila jambo kwa wakati na majira yake, mfano kupanda wakati wa kupanda, kuvuna wakati wa kuvuna, n.k Siku zote ukifanya jambo nje ya wakati wake utaonekana kituko, na matokeo yake ni kutokufanikiwa. Kila jambo huonekana la busara mbele ya wenye hekima likifanyika ndani ya wakati wake, kwa lugha nyingine, "Everything is right at right time". Maana yake ni kwamba ukifanya jambo nje ya wakati hata kama jambo hilo ni jema, litabadilika kuwa baya. Wakati una 'impact' kubwa sana katika jambo lolote.
Kama ni mwombaji au  mdadisi wa mambo muhimu katika taifa letu la Tanzania naamini kabisa unajua ni majira na nyakati gani taifa letu la Tanzania linapitia…. hasa katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu na majira haya tuliopo yanamwitaji kiongozi wa aina gani? Hatuwezi kushindana na majira na nyakati ila sisi binadamu ndio tunapaswa kufuata majira na nyakati. mfano kama leo kuna mvua huwezi kukataa na kusema kuna jua hivyo ukavaa kama unavyovaa wakati jua ni kali.........wewe ndo utaendana na mvua na sio mvua itaendana na wewe. mfano kama ni wakati wa kutokuwa na mabadiliko huwezi kulazimisha mabadiliko......na kama ni wakati wa mabadiliko huwezi kuzuia mabadiliko na kama utaenda kinyume na majira na nyakati uwe tayari na yatakayo tokea.
Tambua majira na wakati ambayo taifa letu lipo.
Tambua kiongozi ambaye kwasasa is right at right time.
Ukifanya jambo nje ya wakati......?
Jitahidi tarehe 25 .10. 2015 Jumapili hii mapema sana asubuhi Ukapige kura . Mungu akuongoze.

Joel Elphas.