TAFAKARI LA WIKI TAREHE 9/8/2015
LENGO LA
MUNGU KUTAKA UJUE UMUHIMU WAKUTAMBUA NAFASI YAKO YAKIROHO KATIKA KAZI/AJIRA
YAKO
Utangulizi:
Moja, Ikusaidie kujua kusudi la
Mungu kukuweka hapo, na mbinu za kutumia wakati wa kutimiza kusudi hilo zaidi
katika upinzani utakao kutana nao.
Esta 4:14 “Kwa maana wewe
ukinyamaza kabisa wakati huu,ndipo
kutakapowatokea wayahudi msaada na
wokovu kwanjia nyingine;ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba
yako;walakini ni nani ajuaye kama wewe
hukuujia ufalme kwaajili ya wakati kama huu?”
U-
Malikia wa Esta haukuwa ni ajira au umaarufu tu, ila ndani yake ulibeba kusudi
la Mungu, kushindwa kuyajua hayo mapena katika nafasi ya kiroho kulimgarimu
Esta wakati wa kulitimiza kusudi, ,Hamani alikuwa ni mpinzani wa Mordekai na
sio Esta, bali upinzani wa Esta ilikuwa ni
Sheria na taratibu za Ufalme.
unapotaka
kutimiza kusudi la Mungu kupitia kazi yako na upinzani ni mkubwa si lazima
utumie taratibu za kazi yako ila nafasi yako ya kiroho ndio itahusika hapo kwa
kutumia mbinu za ulimwengu war oho kuzinyamazisha sheria za kimwili.Esta baadae
sana alipoyajua haya Roho Mtakatifu anayokufundisha sas, ndi akajua kuwa Maombi
na Mfungo vitumike, wakati mwanzo alitaka kutumia sheria na taratibu za kazi.
Pili, ni kukusaidia nafasi yako ya
kiroho kuitawala na kuiongoza kazi yako na sio kazi yako kuongoza nafasi yako
ya kiroho.
Mwanzo 3:9-12 “……Bwana Mungu akamwita Adamu,akamwambia,
uko wapi?...”Ukijua nafasi yako huta ziruhusu sababu
zilizo nje ya sheria na taratibu za aliyekupa nafasi hiyo,zikutoe kwenye nafasi
yako.
Tatu, kukusaidi kuipenda kazi yako
nakufanikiwa katika hiyo,pasipo jarisha kwa wakati huo wengine wanaichukia au
wanaipena, wamefanikiwa hapo au hawajapata mafanikio kulingana na mazingira
yanayo kuzunguka.
Unajua
unaweza ukaitumikia jamii vizuri sana tena wakakupenda sana, lakini Mungu
asipate faida yoyote katika utumishi wako kwa jamii; Fikiri kama Esta
aliitumikia jamii vizuri alafu angeheshimu sheria na taratibu za kazi yake ili
jamii impende, na kusudi la Mungu lishindwe kutimia kupitiayeye wakati Mungu
ametumia gharama nyingi kumuandaa nini kingetokea?
Nne, ni kujua kuwa kama ni Mungu
amekupa kazi hiyo, basi anatake kufanya kazi pamoja nawewe
Tazama Rumi 8: 28 “… katika mambo yote
Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao….,wale walioitwa kwa kusudi lake…”
Mwisho,
kama haupo kazini ujaya jua haya, ipo neema ya Mungu kubwa kukusaidia kurudi
kwenye nafasi yako, tena, kupata faida za kuijua nafasi na kuitumikia. Baada ya
Musa kukaa kwenye nafasi yake Mungu akaanza kuzungumza nae, Musa akwa na uhuru
pia wa kumuuliza maswal, vivyo hivyo Habakuki na wengine wengi
Kutoka 3:2 – 4 “…..;akatazama, na kumbe! kile kijiti
kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, “nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki
hakiteketei.”Bwana alipoona yakwa amegeuka
ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kilekijiti,….”
Inawezekana
wewe ni Mwalimu, Daktari, askari jeshi/polisi, mkulima, mfanyabiashara n.k,
lakini sijui kama umewahi kupata muda wakutamani kujua kazi unayofanya au maisha unayoishi kwa ujumla yana mahusiano gani na nafasi ya kiroho ambayo Mungu amekuumbia na kukuweka kwenye
kazi hiyo ili upitishe kitu cha ufalme wake.Mana nina uwakika kuwa kuulipata
muda wa kumuomba Mungu sana ili upate kazi, na yawezekana unatekeleza majukumu
yakazini vizuri sana tena kwa bidii na kwa kufuata sheria za kazi vizuri.
Lakini
kunakitu kikubwa sana ndani ya hiyo kazi ambacho kama ujakaa kwenye nafasi
yako, unaweza ukafanya kazi vizuri na kutumikia jamii ila usiwe na faida yoyote
katika ufalme wa Mungu mbali na kuwa ulimwomba Mungu na ndiye kakupa kazi hiyo,
si wakristo wengi huwa wanakihitaji hicho hasa wakisha pata kazi.(mfano:Esta
alikuwa malikia, ila Biblia inaonesha sura ya 4 kuwa katika ulimwengu wa roho
umalikia wake ulibeba kusudi la Mungu ambalo yeye alipa shida sana kuelewa
mpaka alipo ijua nafasi yake na kuanza kuitumia….) Na ndio maana wengi
wanafikiri kutimiza kusudi la Mungu ni jambo la kazi za kanisani tu,kama kuwa
mihubiri.
Sasa fuatana na mimi hapa:
1. Inawezekana katika
eneo/mazingira ulipo au kazi hiyohiyo unayofanya ikawa ni kazi sahihi katika
mazingira sahihi na muda sahihi lakini ukashindwa kutimiza kusudi la Mungu kwa
kushindwa kujua nafasi yako au kutokuwa kwenye nafasi katika ulimwengu wa roho.
Mwanzo 3:9-12 “……Bwana
Mungu akamwita Adamu,akamwambia, uko wapi?...”
Kwa
lugha nyepesi, Adamu hakuwa kwenye nafasi
yake, ambayo Mungu anatakiwa kumkuta,au ambayo alimuweka na huwa wanakutana
katika hiyo. Na Adamu anajua nafasi
yake lakini kwa wakati ule anakili hakuwa kwenye nafasi yake kwa sababu Fulani. , ila cha kushangaza
alikuwepo mazingira yale yale ya bustanini kwa muda ule; ndipo utapata picha
kuwa ni nafasi ya kiroho. (jipya hapa…kumbe, kazi ya shetani ni kukutoa
kwenye nafasi yako kwa kutumia
mageuzi ya sheria na sababu zilizofanya ukawekwa kwenye nafasi hiyo, na ili
utoke kwenye nafasi yako inategeme sana mambo mawili (2), moja kujua nafasi yako, pili
kushikilia maelekezo na sheria ulizopewa na aliyekupa nafasi mana ndizo zitakazo
kufanya usitolewe kwenye nafasi hiyo.Nimuhimu pia,ujue kuwa zipo sababu nyingi
za kukutoa kwenye nafasi yako.
Kitendo
cha kushindwa kujua nafasi yako au kutokuwa kwenye nafasi yako ni kuruhusu
kuishi nje ya mipango na kusudi la Mungu. Hata kama upo eneo hilohilo kama ilivyo
kuwa kwa Adamu, tena unaweza hata
kuondolewa katika mazingira sahihi kama adhabu.
2.
Inawezekana unatimiza majukumu yako vizurikazini, kwa kfuata utaratibu
sawa na sheria za kazi zinavyo kutaka, bosi/mwajiri wako anafurahi na watu wanafurahi
lakini katika ufalme wa Mungu usiwe umepata faida yoyote, kwasababu tu
hujatambua au haupo kwenye “nafasi yako kiroho” katika kazi hiyohiyo na
kushindwa kujua nini Mungu anataka kupitia kazi hiyo ukipitishe ili kijenge
ufalme kwake , japo sawa unawatumikia watu vizuri.
Tazama
Mordekai na Esta;
Esta 4:14 “Kwa maana wewe
ukinyamaza kabisa wakati huu,ndipo
kutakapowatokea wayahudi msaada na
wokovu kwanjia nyingine;ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba
yako;walakini ni nani ajuaye kama wewe
hukuujia ufalme kwaajili ya wakati kama huu?”
Nachotaka
ujifunze hapa ni kwamba; Esta kuwa malikia si kwasababu alikuwa mzuri sana japo
ni moja ya kigezo kilicho tumika,tena kama ni msomaji mzuri wa Biblia pamoja na
uzuri wa Esta, bado hakustahili kuwa malikia mana kuna vigezo ambavyo hakuwanavyo,na
hivyo hakutakiwa kuwa malikia. mfano utaifa,kumbuka
alikuwa utumwani ndio maana alikatazwa na Mordekai asitaje kabila wala jamaa
yake.(swala la utaifa ni muhimu
kuliko uzuri,mana ni rahisi mtu wa taifa jingine kumdhuru mfalme au kuruhusu
maadui wa upande wake) Lakini kusudi la Mungu lilimuhitaji Esta awe malikia ili
Mungu apitishe uponyaji wa taifa lake, moja ya sifa kuu, nikuwa, alitakiwa kuwa na uzuri wa umbo
na uso. Kwahiyo utakubaliana na mimi kuwa ilimlazimu Mungu kumuumba Esta katika
uzuri ule nakufanya mazingira ambayo yatazaa matokeo ya kusudi la Mungu kutimia.
Haijalishi alipitia ugumu gani kama uyatima aliokuwa nao ila kuna mchakato
uliokuwa ukiendelea katika ulimwengu wa roho na ulitimia.
Kosa la Esta:
Esta
alikuwa Malikia ambaye hakujua NAFASI yake katika ulimwengu wa roho ila alijua
katika mwili tu, ukiniuliza kwanini, ntakwambia alifuata sheria zote na
taratibu kama impasavyo kwa kuhudumia jamii na jamaa yake vizuri.Kumbuka kuwa
pale Esta alikuwa mazingira sahihi,
na wakati ule ulikuwa sahihi kwa
Esta kuanza swala la ukombozi ambalo ndio kusudi
sahihi,ila hakujua nafasi yake,sijui
uemenielewa hapo.Pili yeye alijua kuwa anatakiwa sana kumtunza mjomba wake
Mordekai” ndio maana tatizo lilipotokea la wao kutaka kuuwawa hakujua nafasi yake kabisa ntakwambia kwanini.
Alicho kifanya ni kumtuliza Mordekai kwa
kumpelekea mavazi; akifikiri
amemaliza mana nafasi hiyo kimwili alikuwa anaijua na alikuwa sahihi kabisa,
lakini hakujua katika ulimwengu wa roho.
Sikia sasa,
moja
ya kazi ya Mordekai ilikuwa ni kumtengenezea Esta mazingira ya kuketi katika
nafasi ile kimwili na kiroho, lakini
Kosa la mordekai, hakumuandalia Esta mazingira ya kuijua nafasi yake katika
nafasi ya ufalme kwa picha ya rohoni, ndio maana ilimsumbua sana Esta, si
kwamba alikusudia kujibizana na Mordekai kwa muda mrefu, hapana yeye alikuwa
anamuelewesha kufuatana na katiba au sheria, mpaka wakati ufahamu wake
umefunguliwa ndipo akajua nafasi yake na akaanza kutumia mbinu za kiroho yani
si maombi tu,bali kwa gia ya mfungo ,wauuh!
Esta mwishoni alipojua nafasi yake katika ulimwengu wa roho alisema mkafunge na
kuomba siku tatu (3), nami ntafunga na watu wangu na nitaingia kwamfalme kinyume
cha sheria.
Nataka
ujue kuwa inawezekana kazi unayofanya ni sahihi,na upo mazingira sahihi na
wakati sahihi, tena nimpango wa Mungu wewe kutimiza kusudi lake kupitia kazi
hiyo.Lakini ni lazima ujue kuwa si
elimu tu imekupa nafasi hiyo,japo nikigezo kimojawapo, lakini kuna mkono wa
Bwana,hivyo nilazima pia ujue nafasi yako katika ulimwengu wa roho, na ukijua
hayo utatimiza kazi hiyo kwa taratibu na sheria za kazi yako,na inapofikia kupitisha kusudi la Mungu kama kuna
kitu kinazuia basi si razima uendane na sheria na taratibu za kibinadamu
zilizowekwa katika ofisi yako, hasa mazingira yale yanayonyima kusudi na mpango
wa Mungu kufanya kazi. (mfano; Esta 4:16…Esta akasema mkaombe…nitaenda kwa
mfalme kinyume cha taratibu).Mana yake asingejua hilo, u-malikia wake
usingekuwa na faida yoyote kwa Mungu.
3.
Ni rahisi sana Mungu kujifunua kwako; lakini nivigumu sana yeye
kujitambulisha kwako kuwa yeye ni nani katika hilo unalofanya au analotaka
ufanye, na yeye atakutambulisha kuwa ni nani kwa jamii unayo ihudumi; pia ni
vigumu kuwa namazungumzo nawewe, hata kukusihi
yakupasayo kufanya kama kutubu kwa kutambua uwepo wake kwako mpaka
utakapo kaa kwenye nafasi yako kiroho katika kazi unayofanya, katika maeneo
ambayo unaweza kuyaona kuwa niyakawaida sana. Kwasababu unapokuwa katika nafasi
yako ni rahisi kuyaona maono yani kuuana kujifunu kwake katika picha ya kiroho
na kumuelewa.
Kutoka 3:2 – 4
“…..;akatazama, na kumbe! kile kijiti
kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, “nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki
hakiteketei.”Bwana alipoona yakwa amegeuka
ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kilekijiti,….”
Umewahi
kujiuliza kwanini Musa alipo kuwa mlima wa Mungu (Horebu) Mungu akuanza
kuzungumza nae mpaka alipo alipogeuka
(katika ulimwengu wa roho)., ndio maana alisema niyaone maono lakini mwanza pamoja
nakuwa aliona kijiti kinawaka na hakiteketei aliona kimwili tu, cha ajabu
Biblia inasema Mungu alioona amegeuka
ndipo alianza kusema nae, yapo mengi utajifunza pindi utakapo jua kukaa
kwenye nafasi yako kiriho katika kazi unayo iona ipo kimwili, moja(1), ukijua nafasi ni rahisi kutubu soma
hapo kwa Musa,Mungu akamwambia mahali hapa ni patakatifu maana yake Musa
alikuwa hajui wakati huo na kuambia
ajitakase pale; pili (2), nirahisi
kuanza kuwa na mazungumzo na Mungu; Tatu(3), ni rahisi Mungu kusema yeye ninani hapo katika kazi yako;
nne(4), ni rahisi wewe kumuuliza Mungu kwanini amekuweka hapo
(hata ukitaka kujifanya mbabe na kukataa hiyo kazi usikatae kabala ya kujua
nafasi yako, ukijua nafasi yako ni rahisi kujua nafasi ya Mungu hapo na
kumuhoji maswali.)ni mbaya sana kukataa kazi sehemu Fulani kama hujajua nafasi
yako hapo na ya Mungu kwako kuwa hapo, tena itakgharimu.
4. Njia mbili zitakazo kusaidia
kuijua nafasi yako au kurudi kwenye nafasi yako
Moja;
Neema ya Mungu ikusaidie Ugeuke (Kutoka
3:3 na Habakuki 2:1)
Unajua
ni vigumu sana kujua uwamuzi alio uchukua Musa kusema natageuka, au Habakuki
kusema name nitasimama kwenye zamu yangu, ni uwezo wa kufanya maamuzi na
kuchukuwa hatua kwa kuitumia ile neema iliyo juu yako. Ndipo damu ya mwana
kondoo inakutakasa na kukupa fulsa ya kumuona Mungu.
Pili;
kupitia mafundisho (neno la
Mungu)kupitia watumishi wake kwa Roho mtakatifu(Esta 4:1-17).
Unaweza
kujifunza pamoja nakuwa palikuwa na ugumu mkubwa sana, ila nguvu ya Mungu ndani
ya Mordekai ilikuwa inamlazimisha mordekai kumpa elimu Esta ili ajue na fasi
yake, japo kosa ni la Mordekai kama mtumishi alimuandaa Esta katika nafasi ya
mwilini na kujisahau eneo la rohoni.Ila swala ni kujitahidi sana moja watumishi
wa Mungu kufundisha na kuandaa watoto katika hali zote, wazazi pia.AMEN
Daniel
Mwaitnga.
Tuombe:
Mungu
asante kwa ajili ya sadaka ya damu ya Yesu kristo, ambayo kwahiyo,
umetustahilisha kuwa wana wa urithi wako wenye haki yakujua siri za urithi wetu
katika ufalme wako,hata kutupa kupokea Roho Mtakatifu katika maono haya,ili
atufundishe sisi,tukujue,tukupende na kuwa na utumishi wenye faida mbele zako
na kuona raha ya kuokolewa.Tujalie sasa kufunguliwa fahamu zetu ili tupate
kuelewe na maandiko kwa uponyaji wa roho,nafsi na miili yetu.amen
Moja,
usipojua nafasi yako kiroho katika kazi unayofanya,ni dhahiri kuwa katika
mazingira uliyopo na muda husika wengine wanaweza kufanikiwa hapo hapo ila wewe
usifanikiwe, au kazi hiyi hiyo unaweza ukaichukia wakati wengine wanaifurahia.
Pili,
kukusaidia kujua kuwa,unatakiwa kuiweka kazi yako au ajira yako ndani ya nafasi
ya kiroho, nasio nafasi ya kiroho kukaa ndani ya kazi. Yani maamuzi ya mbinguni
yaendeshe kazi yako nasio kuruhusu kazi yako kuendesha maamuzi au utawala wa
mbinguni.
Tatu, Mungu anataka ujue mahusiano ya nafasi
ya kazi yako duniani katika nafasi yako kiroho mana anaposhuka kwenye kazi au
ajira yako huketi kwenye nafasi yako ya kiroho.
Mwisho,
Mungu anataka ujue kuwa, ajira au kazi unayofanya si kwaajili ya kukupa
mahitaji yako tu,ila ni sehemu makusudi
kabisa ya mazingira anayoyatumia kama mpango wa wewe kutimiza kusudi
lake.
Kanuni
za Mungu zipo wazi na zina weza kutambulika ata baada ya miaka mingi; ukiona
amekusomesha muda mrefu, si kwa sababu ni sheria kusoma,ila kwasababu muja ya
makusudi atakayo yapitisha kwako yatatumia njia ya elimu hiyo uliyo nayo
Ni
muhimu kuijua nafasi yako ya kazi kiroho, mana ni rahisi Mungu kukufanikisha
kwa sababu anajua unajua nini unafanya na katika mafanikio hayo kama mkristo
nae kusudi lake litafanikiwa kwa kiwango gani.