MAMBO YA KUFANYA KABLA UJACHUKUA MAAMUZI YA MWISHO KWA JAMBO AMBALO LINAKUTESA/LIMEKUCHOSHA KWA KUSHINDWA KULIPATIA MAJIBU KWA MUDA MREFU.
Bwana asifiwe!!
Kutokana nakuwa tuna MWILI na DAMU, huwa tunahisi MATESO/MAUMIVU hasa, nyakati ambazo tunapitia mambo magumu sana,ambayo mara nyingi tunahisi yamezidi IMANI zetu,nyakati hizi kwetu tunakuwa wapweke na kama tupo katika jangwa, kukosa kuwa na sababu au/na majibu tunayo yataka ya tunayopitia kuna tupa kuumia,kusononeka,kunung’unika na hatua inayobaki ni kukata tama kabisa,
Somo la leo ni mambo 3, yatakayo INUA IMANI yako na KURUHUSU USONGE MBELE; kukwambia kuwa katika mapito hayo Bwana yupo hapo,haijarishi wangapi wana kupenda au wanakuchukia kutokana na unachopitia, MFANYE YESU KUWA TEGEMEO LAKO, yani HAKUNA JIBU LOLOTE UNALO TAMANI, LITAPATIKANA NJE YA MIKONO YA BWANA hatakama limechelewa.
Mf: hujawahi kusikia au kuona mtu anaamua kutoa rushwa ya ngono ilimradi tu, apate kazi, mana ni miaka mingi amekaa bila kazi, na jambo hilo lilikuwa mateso kwake. Ni rahisi kumjadili au kumcheka ilia ukweli ukifunuliwa siri ya yeye kufanya hivyo, unaweza muhurumia mana hakuwa na msaada hasa maarifa ya IMANI nyakati hizo zaidi ya kupata anachotaka..madhara yake ni makubwa sasa zaidi ya uwamuzi aloamua kuufanya.
MAMBO YA KUFANYA:
MUHIMU SANA: Usifanye uwamuzi wowote kwa majira haya hatarishi na ya maumivu kwako, kwa kukosa unacho taka kwa muda mrefu, ila tumia muda huu sasa kutulia katikati ya marafiki ambao si kwazo kwako, mazingira mazuri na ya haki kwako japo kwa wakati fulani ili ikusaidie…(Zaburi 1:1-4).
A. KUMSIHI ROHO MT. AKUPE UPENYO UKUMBUKE MAAGANO ULIYO WAHI KUFANYA KWA KUJUA AU KUTO KUJUA YALIYO MEMA AU MABAYA.
Moja ya mambo yanayo wafunga watu kukaa kwenye mateso ya muda mrefu yasiyo na majibu ni Agano, mara nyingi watu huweka maagano kama utani na wakati mwingine pasi kujua; kujua agano ni jambo linalofanya mtu kuvumilia jambo hata kama jambo hilo majibu yake hayapatikani au yamechelewa, pia linakupa njia ya kutoka ktk ugumu huo kwa haraka au wepesi zaidi. Liwe ni agano zuri au baya ambalo umeweka kwa kujua au kuto kujua ni muhimu nyakati hizo kujua mana ni njia ya kutoka kwa wepesi sana. Kuna mateso yana kutesa au yamekuchosha na hupati majibu, ila umesahau agano uliloweka.
KUTOKA 32:10-12. Mungu alichoshwa sana na wana waizraeli, KUCHOSHWA kulimpelekea kuwa na HASIRA, hasira ilimfanya afanye MAAMUZI MAGUMU sana, lakini RAFIKi yake (Musa) alimsihi maamuzi ya kufanya kwa kumkumbusha AGANO, kisha Bwana akasamehe,akasahau, akaghairi.
B. KUOMBA TOBA INAYO LENGA AGANO HILO ULILO FANYA KWA KUJUA AU KUTO KUJUA, ILI KULIVUNJA KWA AGANO {JIPYA} LA DAMU YA YESU KRISTO,
Ni rahisi sana kupata majibu yetu kama kuna maagano hasa yale mabaya ambayo yalifanyika kipindi cha nyuma na nyakati hizi ukumbuki, na unakuta kinachokutesa sasa ni matokeo ya agano lile. Tuna weza weka maagano kwa namna ambayo tulijua au hatukujua, unapofika kwenye nyakati kama hizo omba toba juu ya agano hatakama ume likumbuka au la, swala toba yako ilenge agano, ambayo ni kifungo kikubwa sana katika maisha ya mtu.
C. MBALI NA AGANO, KUJUA SABABU ILIYOFANYA UKUTANE NA JAMBO LINALO KUTESA SASA, NI MLANGO WA KUTOKA KWA HARAKA KAMA NJIA ZA MWISHO.
Muhimu sana kufikiri sababu za jambo hilo kukusumbua na kuzijua njia za kutatua kwa kurudia upya namna yakupata hatima njema. Sababu na njia hizi zitakusaidia sana kuto kufanya maamuzi mabaya juu ya swala hilo ambalo limekutesa kwa muda mrefu na kukupa njia nyepesi ya kupata jibu.
@Daniel Mwaitenga.